Huduma za mtandao zilikatizwa na shule zilifungwa kwa siku ya pili mfululizo katika mji ulio karibu na mji mkuu wa kifedha wa India Mumbai siku ya Jumatano, wakati maandamano ya madai ya unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wawili wenye umri wa miaka minne yakizidi, vyombo vya habari vilisema.
Maandamano hayo huko Badlapur, yapata kilomita 50 (maili 31) kutoka Mumbai, yanakuja huku kukiwa na maandamano ya nchi nzima juu ya ubakaji na mauaji ya daktari mwenye umri wa miaka 31 katika mji wa mashariki wa Kolkata.
Waandamanaji waliokuwa na hasira walifunga njia za reli kwa saa kadhaa siku ya Jumanne, wakitaka haki itendeke kwa watoto hao, wakirejea maandamano kama hayo nchini kote ya madaktari na makundi ya wanawake.
Mamlaka ziliamuru shule zifungwe na huduma za mtandao zilisitishwa kwa siku ya pili ili kuzima mikusanyiko au maandamano yoyote, kituo cha habari cha ABP kiliripoti.
Waziri Mkuu wa Maharshtra Eknath Shinde alisema kesi hiyo itasikizwa katika mahakama mapema,Shinde alisema Jumatano kuwa maandamano hayo yalichochewa kisiasa.
Maharashtra, jimbo tajiri zaidi nchini India, lina uchaguzi wa majimbo uliopangwa baadaye mwaka huu, na Chama cha Bharatiya Janata cha Waziri Mkuu Narendra Modi kinakabiliwa na vita vikali kutoka kwa muungano wa pamoja wa upinzani.
Vyama vya upinzani katika jimbo hilo vimeitisha mgomo wa serikali mnamo Agosti 24, mbunge wa Congress Varsha Gaikwad alisema wakati wa maandamano huko Mumbai Jumatano.