Tukiwa bado tupo kwenye headlines za Uchaguzi 2015 hivi karibuni kumekuwa na taarifa zilizoenea kuhusu vijana waliopatikana katika mikoa kadhaa kusimamia kura au masanduku ya Uchaguzi Mkuu 2015 katika kila jimbo.
Sasa leo Sept 29,2015 ripota wa millardayo.com & Amplifaya alikutana na Mkurugenzi wa huduma za kisheria wa tume ya Uchaguzi, Emmanuel Kawishe kupata majibu sahihi kuhusiana na taarifa hizo..’Hakuna watu walioteuliwa kwenda kusimamia masanduku na tume itaanza rasmi kuwateuwa kuanzia tarehe 26 mwezi wa tisa sasa hivi tume imeanza mafunzo mpaka tarehe 3 mwezi wa kumi tunatoa mafunzo kwa usimamizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na wasaidizi wao tutaenda kwenye kata pia tutaenda kwenye vituo kwa hiyo hao ndio tume itatoa mafunzo kwao – Emmanuel Kawishe
‘Sheria inakataza kwamba haruhusiwa mtu yoyote kupiga kampeni siku ya uchaguzi wala haruhusiwa mtu kuja na nguo ya chama chochote katika chumba cha kupigia kura kwa hiyo wewe njoo na nguo za kawaida na kadi yako ya kupigia kura basi wasimamizi watakupa maelekezo ya kila kitu‘ – Emmanuel Kawishe
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE