Mwimbaji mahiri wa Nigeria Sarah Aderibigbe, almaarufu Ayra Starr, ametangaza kwamba hapendi kutajwa kuwa Msanii Bora wa Kike wa Mwaka na waandaaji wa Tuzo za Headies.
Kulinga na Daily post imeripoti kuwa mtangazaji mwenza wa Tuzo za 16 za Headies, mwigizaji Osas Ighodaro, alitangaza katikati ya onyesho hilo kuwa sherehe hiyo imefikia tamati, huku kukiwa na vipengele takriban 13, kikiwemo cha Msanii Bora wa Kike, bado havijatolewa.
Baadaye waandaji walitangaza washindi wa vipengele hivyo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.
Akijibu kupitia ukurasa wake wa X siku ya Jumatatu, Ayra Starr aliandika: “Sitawahi kushukuru kwa kushinda kitengo ambacho hata hakikustahili kutangazwa jukwaani. Msanii bora wa kike na beans? Tunafanya kazi kwa bidii, kila mmoja wetu! Nimemuona Tiwa akirekodi nyimbo nne zilizovuma kwa usiku mmoja. Tems anapumua na anaishi kwa muziki. Hatukustahili uzembe kama huo! Nigeria, hukunilea ili nipambane kidogo.”