Msichana mwenye umri wa miaka mitatu ameokolewa kutoka kwenye kifusi cha jengo lililoporomoka katika mji wa Izmir magharibi mwa Uturuki, siku tatu baada ya tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7 katika kipimo cha Richter kutokea katika Bahari ya Aegean.
Mpaka sasa tetemeko hilo limesababisha vifo vya watu wasiopungua 85.
Waokoaji walimtoa msichana huyo, Elif Perinçek, kutoka kwenye kifusi na kumpeleka kwenye gari ya wagonjwa kwa uangalifu wakati wafanyakazi wa dharura wanatafuta watu walionusurika katika majengo mengine manane.
Dada wawili na kaka wa Elif walipatikana wakiwa hai kwenye mabaki pamoja na mama yao Jumamosi, lakini mmoja wa watoto alikufa baadaye. Tetemeko hilo pia limesababisha vifo vya vijana wawili katika kisiwa cha Ugiriki cha Samos.
UWEZO WA KOMANDO WA JWTZ, UTABAKI MDOMO WAZI