Siku ya kimataifa ya Bia inaadhimishwa kila mwaka siku ya ijumaa ya kwanza ya mwezi Agosti, na sherehe ya kimataifa ya mojawapo ya vinywaji vikongwe na vinavyopendwa zaidi na binadamu.
Kwa kuzingatia utamaduni wa karne nyingi, siku hii inaangazia sio tu aina mbalimbali za Bia zinazopatikana bali pia faida za kijamii na kitamaduni za kushiriki kinywaji hicho na marafiki, mwaka huu, siku ya kimataifa ya Bia inaadhimishwa leo tarehe 2 Agosti 2024, na tuna sababu nyingi za kusherehekea.
Ilianzishwa mwaka wa 2007 na Jesse Avshalomov huko Santa Cruz, California, siku ya kimataifa ya Bia hapo awali ilikuwa sherehe ya ndani iliyolenga kuheshimu jukumu la Bia katika maisha yetu, baada ya muda, ilipata mvuto na sasa inaenea ulimwenguni, na matukio au sherehe zikifanyika katika nchi nyingi.
Moja ya mambo ya kusisimua zaidi kuhusu Bia ni utofauti wake wa ajabu, wapenzi wa kinywaji hicho wakiwa na uwezo wa kuchagua aina mbalimbali za kinywaji hicho, aina ya kwanza ni Lager: inajulikana kwa ladha yake safi na huchachushwa kwenye halijoto ya baridi, inasifika kwa sifa yake ya dhahabu n.k.
Aina nyingine ni Ale: hii huchachushwa kwenye halijoto ya joto zaidi, na kutoa aina mbalimbali za ladha, mara nyingi ina ladha kali, aina nyingine ni Bia ya ngano: hii imetengenezwa kwa sehemu kubwa ya ngano pamoja na shayiri, bia za ngano zinajulikana kwa mwanga wake, mwonekano wa mawingu na ladha ya kuburudisha.
Nyingine ni Bia kali: hizi hutengenezwa kimakusudi ili ziwe na ladha ya siki au tindikali, huku aina ya tano ni Bia Maalum na Ufundi: hii hutengenezwa kwaajili ya upekee fulani kwa kuongezewa vitu kuwa bora, faida za kinywaji hiki ni kuunganisha jamii, umuhimu wa kitamaduni, manufaa ya kiafya kama kuboresha moyo n.k