Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwafuata Wananchi na kusikiliza pamoja na kutatua kero zao na amewaelekeza Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanapokea taarifa za Wakuu wa Wilaya kuhusu ziara zao kwa Wananchi.
“Kuanzia sasa Wakuu wa Mikoa wote na Wakuu wa Wilaya washuke chini kusikiliza kero za Wananchi, asilimia 45 ya Wakuu wa Wilaya hawafanyi kazi kabisa, hawasikilizi kero za Wananchi, kwahiyo tunataka kila mmoja afanye kazi ili tuweze kutimiza malengo ya Watanzania, malengo ya Chama cha Mapinduzi na malengo ya Rais wetu”
“Niwaombe Watumishi wenzangu kuwa sasa tunairejesha Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa Wananchi, maana yake tunataka kufanya kazi hasa ili tuweze kufanikiwa na malengo ya Mh. Rais yaweze kufanikiwa, hivyo lazima tufanyekazi usiku na mchana hakuna namna, Wizara yetu tunaisogeza kwa Wananchu, tutasikiliza kero za Wananchi”