Kuelekea siku ya Vipimo Dunia, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewashauri watoa huduma za kijamii pamoja na wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wamehakiki vifaa vyao katika shirika hilo ili kujihakikishia kama vifaa hivyo vinakidhi ubora wa viwango vya kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 16,2022 Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Metrolojia kutoka TBS, Stella Mroso amesema kuwa maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika jijini MWANZA ambapo amewakaribisha wafanyabiashara pamoja na wananchi wote kuhudhuria maadhimisho hayo ili kujipatia elimu sahihi ya vipimo.
Aidha amesema wafanyabiashara wengi hukosa fursa za kufanya kazi na mashirika pamoja na taasisi kubwa za kimataifa kwa sababu ya kukosa uthibitisho wa ubora wa viwango wa vifaa wanavyotumia hali ambayo pia inalikosesha taifa mapato.
“Wafanyabishara na watumiaji wa bidhaa zinazohusiana na vipimo ni vyema wakafuata hatua hizo ili kuendelea kuimarisha ubora wa viwango unaotakiwa kimataifa”. Amesema Bi.Stella.
Kwa upande wao afisa vipimo mkuu Joseph Mahilla pamoja na afisa vipimo mwandamizi Joseph Kadenge wamesema kuwa dunia iko katika mapinduzi ya teknolojia kidigitali hivyo nchi nayo inapaswa kuenda sambamba na mabadiliko yenye tija katika uchumi wa nchi.
Meneja wa Metrolojia kutoka TBS, Stella Mroso akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi za Makao Makuu ya TBS leo Mei 16,2022 Jijini Dar es Salaam Afisa Vipimo Mwandamizi (TBS), Bw.Joseph Kadenge akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi za Makao Makuu ya TBS leo Mei 16,2022 Jijini Dar es Salaam Afisa Vipimo Mkuu (TBS) Bw.Joseph Mahilla akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi za Makao Makuu ya TBS leo Mei 16,2022 Jijini Dar es Salaam