Kampuni kubwa ya usafirishaji nchini Tanzania ya SILENT OCEAN ambayo husafirisha mizigo kutoka China, Uturuki na Dubai kuja Tanzania, imeanza kuwapokea Wafanyabiashara mbalimbali wa Tanzania wanaoingia China ikiwa ni wiki zisizopungua nne toka China itangaze kuanza kufungua mipaka yake na kuruhusu Wageni toka nje baada ya lockdown ya miaka.
Mmoja wa Wafanyabiashara wa Tanzania waliopokewa hivi karibuni ni Mmiliki wa Maduka ya VUNJA BEI Fred Ngajiro maarufu Fred Vunjabei ambaye pia ndiye mwenye tenda ya kutengeneza jezi za Timu ya Simba.
Katika Kampeni yake ya sasa iitwayo TUKUTANE CHINA, Kampuni hii yenye uzoefu wa miaka 19 ya usafirishaji mizigo imeahidi kuwasaidia Wafanyabiashara Watanzania na kuwafanyia wepesi kwenye usafirishaji wa mizigo yao ili kurejesha uchumi wa biashara zao ambao umeathirika kwa kiasi kikubwa kutoka na China kufunga mipaka yake kwa muda wa miaka mitatu.