Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Tulia Akson ameahirisha kikao cha Bunge Jumatatu Aprili 25, 2022 kufuatia kifo cha Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa (CCM), Irene Ndyamkama kilichotokea April 24,2022 katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha mkoani Pwani alikokuwa akipatiwa matibabu.
Dk Tulia amesema mwili wa mbunge huyo unatarajia kuagwa na wabunge Jumatano Aprili 27, 2022 katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.
“Aliugua hgafla akiwa safarini kuelekea Dar Es Salaam ikalamika kukimbizwa Hospitali na kwamujibu wa kanuni za bunge tunapofiwa na mbunge mwenzetu wakati wa mikutano ya bunge siku ya kazi kunakuwa hakuna kikao cha bunge mwili utaletwa bungeni siku ya Jumatano tarehe 27 Aprili,2022 na atazikwa Ijumaa tarehe 29 mkoani Katavi”- Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson