Club ya Simba SC kupitia kwa CEO wao Barbara Gonzalez leo imetangaza kuomba ulinzi kwa Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini wakiwa wanaelekea Afrika Kusini katika mchezo wa marudiano wa robo ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates.
Maamuzi hayo yamekuja ikiwa ni siku mbili zimepita toka Kocha Msaidizi wa Orlando Pirates Mandla Ncikazi kuituhumu Simba SC kwa mambo kadhaa ikiwemo Mapokezi mabovu, hakuna ukarimu na madai ya VAR kutofanya kazi.
VURUGU: RC KIGOMA APIGA MARUFUKU GARI HIZI KAMA MCHOMOKO, ‘UPAKIA ABIRIA HOVYO’