Zikiwa zimebakia siku 10 kabla ya kujitupa uwanjani kupambana na mahasimu wao wa jadi – Yanga, klabu ya Simba imeamua kuhamisha kambi yao kwenda nje ya nchi.
Msafara wa kwanza wa Simba SC
umeondoka jana jioni kwenda
Johannesburg, Afrika Kusini kuweka
kambi ya wiki na masiku kadhaa kwa ajili ya kujiandaa na mpambano dhidi Yanga SC Oktoba 18, mwaka huu
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Msafara huo unaojumuisha wachezaji
ambao hawako timu ya taifa, Taifa
Stars- umeondoka kwa ndege ya Fast
Jet ukiongozwa na kocha
Mkuu,Patrick Phiri.
Simba SC itakuwa itafanya mazoezi hadi Oktoba 17 itakaporejea Dar
es Salaam, ikiwa ni siku moja kabla ya
mechi.
Wacheaji waliopo timu ya taifa ya
Tanzania, Taifa Stars wataondoka Dar
es Salaam baada ya mechi na Benin
Jumatatu.
Aidha pia Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi hatakwenda kabisa Afrika Kusini kwa sababu atakuwa kwenye majukumu ya kimataifa kwao,
Uganda.