Wiki kadhaa nyuma mfanyabiashara mkubwa na maarufu Tanzania Mohamed Dewji aliweka wazi dhamira yake ya kutaka kuinunua klabu ya Simba na kuwekeza bilioni 20 kwa ajili ya klabu hiyo, Dewji lengo lake ni kununua hisa asilimia 51 za klabu ya Simba na kuiwezesha ifike mbali.
Taarifa za Dewji kutaka kuinunua klabu hiyo zilitoka wiki kadhaa nyuma na kuthibitisha kuwa tayari ameeleza dhamira ya lengo lake hilo kwa Rais wa sasa wa klabu ya Simba Evans Aveva na kumwambia aandike barua rasmi ya kuomba kuuziwa klabu hiyo, Stori za November 4 mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo Ismail Aden Rage ameeleza mtazamo wake kuhusu wazo la Mohamed Dewji, vipi kama angekuwa yeye ndio Rais angefanyaje?
“Tatizo ni kwamba wanachama wetu sisi wanapenda tu vilabu vyao na mashabiki wanapenda kuchangia michango yao kwa kulipa viingilio uwanjani ila tatizo ni kwamba vilabu vyetu havipati udhamini wa maana ila usidhani kama mtu mmoja pekee anaweza kufanya mabadiliko katika mpira hakuna duniani mafanikio kama hayo”>>> Aden Rage
“Kama ningekuwa Rais wa Simba kwa sasa kuhusu suala la mtu kumiliki hisa nyingi katika klabu kwanza ningefanya utafiti wa kuangalia Hispania wanafanya nini, Ujerumani wanafanya namna gani,baada ya hapo ningelipeleka kwa wanachama kwa sababu ile klabu sio ya kwangu”>>> Aden Rage
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.