Klabu ya soka ya Simba inayonolewa na kocha muingereza Dylan Kerr huku msaidizi wake akiwa Selemani Matola imezidi kuingia katika headlines baada ya zile tetesi za muda mrefu kuthibitika rasmi usiku wa November 11, awali kulikuwa na stori za mahusiano yasio mazuri kati ya kocha mkuu wa timu hiyo Dylan Kerr na msaidizi wake Selemani Matola.
Kulikuwa na tetesi nyingi kuhusu mahusiano ya kocha huyo na msaidizi wake kwani inadaiwa iliwahi kufikia hata kutoaminiana wakati mwingine Kerr alikuwa akizungumza na wachezaji wake Matola alikuwa anatakiwa kutoka nje ila hizo zilikuwa stori tu ila maamuzi ya Selemani Matola kuacha kazi ya kuwa msaidizi wa Kerr yamezidi kuthitibika kuwa yote yaliokuwa yanaandikwa ni kweli.
“Ni jambo la muda mrefu, huyu kocha hasikilizi ushauri wangu, imefikia sasa ananichukia na kazi haziendi tena. Sasa nimeona ili kuepusha matatizo zaidi, nimuachie yeye timu. Nimekutana na uongozi, nimewaambia juu ya uamuzi wangu, wakanisihi sana nisifanye hivyo, lakini nikashikilia msimamo wangu. Wakaniambia hata nirudi kufanya kazi timu za vijana, lakini nikawaambia nitajifikiria kwanza” >>>> Selemani Matola
Selemani Matola aliwahi kuicheza Simba kwa miaka kadhaa na baadae kuwa kocha wa timu ya vijana ya klabu hiyo, lakini Matola aliwahi kucheza Kagera Stars kabla ya kuhamia Simba na mwaka 2005 alitimkia Afrika Kusini kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Super Sport United.
CHANZO CHA STORI HII : BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.