Klabu za Ligi Kuu soka Tanzania bara zinazidi kuimarisha vikosi vyao kwa kutumia vizuri siku 14 zilizosalia kabla ya dirisha dogo la usajili la Ligi Kuu soka Tanzania bara halijafungwa December 15. November 30 uongozi wa klabu ya Azam FC ulithibitisha kumsajili golikipa wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Ivo Mapunda.
December 1 ni headlines za usajili kwa upande wa klabu ya Simba ambayo mwezi November ilitangaza kuwatema wachezaji wake wawili wa kimataifa msenegal Pape N’daw na mganda Simon Sserunkuma hivyo wengi walikuwa wanataka kufahamu nani atarithi nafasi za wachezaji hao.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Simba ilitangaza kumpokea kiungo wa kimataifa wa Uganda aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Azam FC Brian Majwega ambapo kiungo huyo aliomba kufanya mazoezi na klabu ya Simba wakati ambao anasubiri kujua hatma ya mgogoro wake baina yake na Azam FC.
December 1 uongozi wa klabu ya Azam FC kupitia kwa afisa mawasiliano wa klabu hiyo Jafari Iddi Maganga amethibitisha kumalizana na Simba, hivyo rasmi sasa Simba imepewa baraka za kumtumia mchezaji huyo na huenda tukamuona katika mchezo wa December 12 baina ya timu hizo mbili.
“Simba wameheshimu kuwa Majwega alikuwa na mkataba na Azam FC walichofanya Simba ni kuja kufanya mazungumzo na Azam FC na kufikia makubaliano baada ya Simba kutumia busara kukaa na Azam na kufikia muafaka, hivyo tumeyamaliza na tunasema ni ruhusa Majwega kwenda kucheza Simba” >>> Jafari Iddi
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.