Simu aina ya iPhone iliyopotea mtoni imepatikana miezi 10 baadae na kurudishwa kwa mmiliki wake ikiwa bado inafanya kazi.
Miguel Pacheco (29) wa Uingereza aliokota simu hiyo mwezi huu kwenye mto Wye na kushea picha kwenye mtandao wa Facebook ili kujaribu kumpata mmiliki.
Alikwenda na simu hiyo nyumbani, akaikausha na kesho yake alianza kuichaji na kushangaa ilikuwa inafanya kazi.
Posti yake ya Facebook ilisambazwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii na hatimaye mmiliki wa simu hiyo Owain Davies (35) alipatikana.
Kwenye kioo cha simu hiyo kulikuwa na picha ya mwanaume na mwanamke, pia kulisomeka tarehe 13 Agosti siku ambayo simu hiyo ilipotea mmiliki wake alipokuwa na wenzake kwenye mtumbwi.