Star wa Singeli ni moja kati ya shindano lililoandaliwa na High Time Marketing and Promotion Co Ltd kwa lengo la kukuza muziki wenye asili ya kitanzania lakini pia kuibua vipaji vya wanamuziki wa singeli kwa kuwaonyesha njia sahihi ya namna wanavyoweza kutumia style hiyo ya muziki kujitengenezea mkwanja.
Katika shindano hilo mshindi atajipatia shavu yafuatayo:-
. Pesa taslimu
. Kusimamiwa mizuki wake chini ya High Time
. Kurekodi album yake ya audio
. Kufanyiwa video tatu zenye viwango vya kimataifa
. Kutangaza muziki wake ndani na nje ya nchi
August 20 2016 ndio uzinduzi ulifanyika katika Wialaya ya Temeke na yataendelea tena August 21 katika Wilaya ya Kigamboni
Hii hapa chini ni moja kati ya video ya washiriki waliopata nafasi ya kupanda on stage..
ULIIKOSA HII YA MSAGA SUMU NA WATU WAKE WA MBAGALA KATIKA KISINGELI