Anaitwa Baby John Musamba (26) alizaliwa huku jinsia yake ikiwa haitambuliki (Jinsia Tata) na anaishi na hali hiyo hadi sasa , inawezekana umeshakutana na clip yake akiwa anaomba kura mbele ya Wajumbe, Baby anasema dhamira yake ni kwenda Bungeni ili kuwasemea wenye tatizo kama lake ambao wengi wamekuwa wakijificha au Familia zao kuwaficha.
“Sina jinsia, sipati hisia za kimapenzi, nilikuwa naumizwa sana kuitwa Jike Dume, wenye tatizo kama langu wako wengi lakini wengi wanajificha, nataka kuingia Bungeni nikawasidie, natamani kupata platform, kuanzisha foundation ili kupaza sauti”-Baby John
Yapo mengi ambayo tumezungumza na Baby John tulipomtembelea nyumbani kwa Kaka yake mbele kidogo ya Fremu kumi Kivule DSM kuhusu maisha aliyopitia tangu anazaliwa hadi sasa..Bonyeza PLAY hapa chini kutazama