Maelfu ya Watu wanaoishi na virusi vya HIV sasa wamepata kilichoitwa ahueni baada ya kutangazwa kwa sindano mpya inayoweza kufanya kazi kwa muda mrefu ambayo watakua wakichomwa badala ya kumeza vidonge kila siku.
Sky News wameripoti kwamba Mashirika ya misaada yamekubaliana na njia hii ya matibabu ya Taasisi ya usimamizi wa dawa nchini Uingereza NHS ambapo sindano hii ina uwezo wa kuondoa makali ya virusi vya UKIMWI kama ilivyo kwa dawa za kawaida za antiretroviral.
Mamlaka hiyo ya NHS imepewa ruhusa ya kuwachoma sindano hiyo Watu elfu kumi na tatu 13,000 wanaoishi na virusi ambapo hii inamaanisha Watu hao hawatohitaji tena matibabu ya kila siku bali watakuwa na sindano mbili tu kila baada ya miezi miwili, hii pia inamaanisha kwamba Watu hao wenye HIV wanaweza kupunguza siku wanazopokea matibabu kutoka 365 hadi siku sita tu kwa mwaka.