Singapore imemnyonga Mwanamke aitwae Saridewi Djamani (45) ambaye alikutwa na hatia ya kumiliki gramu 30 za dawa za kulevya aina ya heroine mwaka 2018.
Kunyongwa kwa Djamani kumefanyika wakati kukifanyika maandamano ya kupinga hukumu hiyo ambapo Mashirika ya kutetea haki za Binadamu yalikuwa yakizishikiza Mamlaka nchini humo kumsamehe Mwanamke huyo yakisema adhabu ya kifo ni ukatili.
Sheria za Singapore zinaruhusu adhabu ya kifo kwa Walanguzi wa dawa za kulevya iwapo watakutwa na heroine ya zaidi ya uzito wa gramu 15 ambapo Mwanamke wa mwisho kunyongwa kabla ya Djmani alinyongwa mwaka 2004.
Singapore ambayo juzi passport yake imetangazwa kuwa ndio yenye nguvu zaidi duniani, ni miongoni mwa Nchi zinazosimamia vilivyo sheria zake ambapo ukiachia hizo za dawa za kulevya, kuna sheria mbalimbali ikiwemo ya kukataza uuzaji na utafunaji wa’chewing gum’ na ya kukataza kula au kunywa kwenye usafiri wa umma