Watoto wadogo wamekuwa katika hatari ambapo mara nyingi tumesikia taarifa za watoto kufanyiwa vitendo mbalimbali vya kikatili na watu wazima.
Taarifa kutoka katika mitandao ya Nigeria imesema watoto wadogo wawili ndugu, mmoja mwenye umri wa miaka sita na mwingine miaka nane wamebakwa na mwanaume ambaye amewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mama yao.
Mtu huyo, Terkula Iorpuur mwenye miaka 32 aliyekuwa akijishughulisha na kazi za ujenzi, aliripotiwa kituo cha Polisi cha ‘B’ Division Police Station na mjomba wa watoto hao ambapo alikamatwa.
Mama wa watoto hao aligundua hali ya utofauti kwa watoto hao ambapo walikuwa hawatembei vizuri.
Mwendesha mashtaka Terzungwe Kajo amesema uchunguzi umeonyesha mshtakiwa huyo ana maamukizi ya VVU.
Kesi hiyo imesogezwa mbele mpaka tarehe 4 Desemba ambapo itatajwa tena na mshtakiwa amerudishwa gerezani.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook