Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya August 25 2016 ni hii kutoka gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Kitwanga aponda ndege mpya ATCL mwanzo mwisho’
#NIPASHE Kitwanga aponda aina ya ndege mpya ATCL, asema hazina mwendo na zinatoka kampuni ndogo ya mtu binafsi pic.twitter.com/KvNmfKhSLW
— millardayo (@millardayo) August 25, 2016
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga jana aliponda aina ya ndege mpya zilizonunuliwa na serikali kutoka Canada kwa ajili ya kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
Kitwanga alisema ndege hizo si tu hazina mwendo, lakini pia ilikua ni ajabu kununuliwa kwa fedha taslimu wakati duniani kote ndege hununuliwa kwa kulipa kidogo kidogo wakati mteja akiendelea kuzitumia.
Serikali imelipa kwa Bombardier Aerospace fedha za ndege mbili za Q400 zinazotumia injini ya pangaboi zenye uwezo wa kubeba abiria 70.
Kitwanga ambaye ni mbunge wa Misungwi (CCM), alieleza kushangazwa na kitendo cha serikali kununua ndege hizo ambazo amesema zimetoka katika kampuni ndogo ya mtu binafsi, na kuhoji ubora wake. Aidha Kitwanga alisema Tanzania itakua mteja wa kwanza wa ndege hizo.
Hata hivyo kwa mujibu wa mtandao wa kompyuta wa wikipedia, kampuni hiyo imetengeneza zaidi ya ndege 1,000 za aina hiyo tangu ianzishwe mwaka 1984, na inatarajia kuwa imetengeneza jumla ya ndege 1,192 ifikapo mwisho wa mwaka huu.
Kitwanga alisema hayo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipokutana na ATCL, na Mamlaka ya Usafiri wa wa Anga (TCAA) mjini Dodoma.
Source: Nipashe
Unaweza kupitia habari nyingine kubwa kutoka kwenye magazeti ya Tanzania
#MWANANCHI Hofu iliwakumba wakazi na wafanyabiashara Mbagala Dar baada ya kushuhudia polisi wakifanya mazoezi pic.twitter.com/Smb7x6pjA8
— millardayo (@millardayo) August 25, 2016
#MWANANCHI NHC imetoa notisi ya kuhama ofisi za wizara 11, idara 29 na jengo la Bilicanas kutokana na deni la pango pic.twitter.com/V88YB9Teqa
— millardayo (@millardayo) August 25, 2016
#MWANANCHI Polisi yapiga marufuku mikutano ya ndani ya vyama vya siasa kwa kile kinachoelezwa kuwa inachochea vurugu pic.twitter.com/FUaEHFirpz
— millardayo (@millardayo) August 25, 2016
#MWANANCHI TAKUKURU imeanza kuchunguza ufisadi wa zaidi ya bil 1.2 ktk kampuni ya Tanganyika Coffee Curing Moshi pic.twitter.com/Z1t7oXKFAT
— millardayo (@millardayo) August 25, 2016
#MWANANCHI NHC kuanzisha miradi mikubwa ya ujenzi Dodoma, tayari imejenga nyumba 153 na kuziuza 56 pic.twitter.com/DS5Ozmbv8S
— millardayo (@millardayo) August 25, 2016
#MWANANCHI CAG kutembeza bakuli ili kufikia malengo ya kuwasaidia watumishi 35 wa ofisi yake wanaoishi na VVU pic.twitter.com/zneHmI0kVZ
— millardayo (@millardayo) August 25, 2016
#NIPASHE Kitwanga aponda aina ya ndege mpya ATCL, asema hazina mwendo na zinatoka kampuni ndogo ya mtu binafsi pic.twitter.com/KvNmfKhSLW
— millardayo (@millardayo) August 25, 2016
#JamboLEO Mengi aomba siku 14 ili ajieleze kwa nini asifungwe jela kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya kulipa bil 1.2 pic.twitter.com/sRQp05HwL6
— millardayo (@millardayo) August 25, 2016
#JamboLEO Watumishi zaidi ya 100 wizara ya ulinzi ambao si askari warudishwa ofisi ya Rais, utumishi na utawala bora pic.twitter.com/gtbXAtITtd
— millardayo (@millardayo) August 25, 2016
#JamboLEO Wajumbe kamati ya bunge ya miundombinu wavutana kupata mtendaji mkuu ATCL wengine wataka atoke nje ya nchi pic.twitter.com/pl1rEdXAjh
— millardayo (@millardayo) August 25, 2016
#JamboLEO Halmashauri ya jiji Dar kuwaondoa wapiga debe na madalali wanaowasumbua abiria ktk kituo cha mabasi ubungo pic.twitter.com/2UTQzPAu12
— millardayo (@millardayo) August 25, 2016
#MTANZANIA Viongozi wa serikali, dini, vyama vya siasa wakutana kwa saa 10 kujadili mambo mbalimbali ikiwemo UKUTA pic.twitter.com/GqlPYzSnCo
— millardayo (@millardayo) August 25, 2016
ULIKOSA ALICHOKIONGEA KIGUNGE NGOMBALE MWIRU KUHUSU CHADEMA NA SERIKALI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI