Hatimaye aliyekuwa Mwenyekiti wa muda Bunge Maalum Pande Ameir Kificho leo ameachia wadhifa wa kiti hicho na kumkabidhi jukumu hilo Mwenyekiti wa bunge hilo la katiba Samwel Sitta na Makamu wake Samia Suluhu Salehe ili kuongoza mchakato wa kuijadili rasimu ya katiba.
Kabla ya kukiachia kiti hicho AMEIR KIFICHO alianza kwa kuwaapisha viongozi hao na baada ya kukamilisha zoezi la uapishaji Pandu amelihutubia bunge hilo na kuwataka viongozi hao kuusimamia ipasavyo mchakato huo ili kupata
katiba mpya itakayowaondolea umaskini wananchi huku ikidumisha Muungano wa Tanzania unaotimiza miaka 50 mwaka huu.
Baada ya kukalia kiti hicho, SITTA ametumia fursa hiyo kushukuru utendaji wa mwenyekiti wa muda na kuwataka wajumbe kuanza kufuata kanuni zilizopitishwa na bunge hilo na kwamba hatosita kumchukulia hatua mjumbe atakayeenda kinyume na taratibu zilizopo.
Baada ya tamko hilo kazi ya kuanza kuwaapisha wajumbe ilianza huku Mwenyekiti Mstaafu PANDU AMEIR KIFICHO akifungua pazia la zoezi hilo litakalofanyika mfululizo kwa siku tatu.