Floyd Mayweather amekataa kumkosoa Diddy kuhusu madai yake ya unyanyasaji wa kingono yanayomhusu hivi sasa na yanayoshika kasi kwenye mitandao.
Bondia huyo mstaafu wa kulipwa alikuwa akitokea kwenye The Pivot Podcast iliyoandaliwa na Channing Crowder wa zamani wa NFL Stars, Fred Taylor na Ryan Clark wakati mada mojawapo ya mwanamuziki huyo wa Hip Hop iliyomchafua ilipoibuka.
“Sitazungumza vibaya kuhusu P. Diddy,” Mayweather alisema. “‘Kwa sababu bado ni mtu Mweusi ,makosa hutokea. Na siwezi kusema ikiwa ni makosa au la, lakini mambo hutokea katika maisha.
Biashara ya P. Diddy ni biashara ya P. Diddy. Sio kazi yangu au ya mtu mwingine yeyote kwenda kwenye mtandao na kumsema na kumpiga mawe mwanaume kama yeye.
“Mtazamo wangu juu yake ni: sio kazi yangu. Sidhani kama ni sawa hata kidogo na sikubaliani nayo. Hata kama hilo lingetokea kwa binti yangu, ningeumia lakini hilo ni chaguo ambalo binti yangu alifanya.”
Baada ya maelezo ya Floyd, Clark aliingilia kati na kusema: “Ikiwa mtoto wako anatuhumiwa kwa mambo ambayo Diddy alishutumiwa, nitamwamini mwanangu katika kile anachosema lakini ninamchunguza kuhusu hilo.
“Na kwa upande mwingine ambao tunapaswa kuwa waangalifu sana, hasa tunapozungumzia wanawake, ni kwamba ikiwa mambo hayo ni ya kweli, huo haukuwa uamuzi wao; hilo ni jambo ambalo walifanyiwa.