Kampuni ya michezo ya ubashiri ya SportPesa Tanzania leo Alhamisi ya January 5 2018 ikiwa ni siku mbili zimepita toka kampuni yao ijitoe kudhamini michezo mbalimbali nchini Kenya, leo mkurugenzi wa utawala na utekelezaji wa SportPesa Tanzania Abbas Tarimba ameongea na waandishi wa habari.
Tarimba ameongea na waandishi wa habari leo dhumuni kubwa ikiwa ni kutoa hofu kwa mashabiki soka nchini na wateja wa SportPesa na kueleza kuwa maamuzi hayo ya SportPesa yamefanyika kwa timu ya ndani za Kenya pekee na wala timu zilizodhaminiwa na SportPesa nje ya Kenya hazitaweza kuathirika maaamuzi hayo.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya SportPesa nchini Kenya Ronald Karauri Jumanne ya January 2 2018 alitangaza kuwa kampuni yao imefuta udhamini wa michezo yote na kwa timu zote nchini Kenya baada ya kuongezewa tozo la kodi kutoka asilimia 7.5 hadi 35.
Simon Msuva amerudi Tanzania leo, alichozungumza kipo hapa