Mtandao wa skype ambao umekua ukitumika na watu mbalimbali duniani kama njia ya kuwasiliana huku kila mmoja akipata nafasi ya kumuona mwenzake wa upande wa pili kwa njia ya video, umepata kitu kingine kipya kitachorahisisha mawasiliano zaidi. (Skype Translator)
Unaambiwa kabla mwaka 2014 haujaisha, Microsoft wana mpango wa kuileta hii huduma itumike na kila mtu, yani ni application ambayo inaweza kutafsiri lugha mbalimbali na kuwawezesha watu wanaowasiliana kwa lugha tofauti kusikilizana papo kwa papo mfano mtu anaeongea Kijerumani akaongea lugha hiyo lakini wa upande wa pili akawa anamsikia kwa Kiingereza.
Wanasema hii imekuja kuvunja mipaka ya matumizi ya lugha, sasa itakuwezesha kuwasiliana na kuelewana na yeyote ulimwenguni kwa sababu inayachukua uliyozungumza na kuyaweka kwenye lugha uliyochagua, sauti inakua ileile ya kiume kama wewe ni Mwanaume au ya kike kama wewe ni Mwanamke.
Kitu kimoja ambacho sijakifahamu ni kama Kiswahili kitafanya kazi ndani yake, unaweza kutazama hii video hapa chini ili kuipata zaidi.
Ili niwe nakutumia kila taarifa inayonifikia jiunge na mimi kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.