Jumamosi ya October 1 2016 soka la Tanzania litaingia katika historia mpya kutokana na mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga na Simba Jumamosi hii uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mashabiki wataanza kuingia katika uwanja huo kwa tiketi za electronic.
Mashabiki watalazimika kuingia uwanjani kwa Smart Card maalum ambazo zimeanza kutolewa bure toka jana lakini unatakiwa kuziwekea hela ndio uanze kununua tiketi yako ya mechi, waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Nape Moses Nnauye ametoa kauli kuhusu mfumo huo na utatuaji wa changamoto.
“Kuelekea mechi ya kesho ya Simba na Yanga mfumo huu wa tiketi za kielectronics ni mpya kwa watanzania, kumekuwa na malalamiko kuwa mambo hayaendi sawa mtaani kwa watu wanalalamika kuwa watu hawapati kadi, kama vile kuna hisia kuwa mambo hayaendi sawa, kiukweli kwa gharama yoyote ile siwezi kukubali mfumo huu kuanguka”
GOALS: TP Mazembe vs Yanga August 23 2016, Full Time