Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezungumza mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli akielezea taratibu za mazishi ya Hayati benjamin William Mkapa ambapo tunawajibu wa kumuombea Hayati Mkapa.
“Jambo hili au tukio hili halivumiliki,ni jambo la huzuni,ni tukio ambalo kutuwezi kuzisahau kwa sababu mpendwa wetu amefanya kazi kubwa sana nchini,na kila Mtanzania anajua,na hayo yamethibitishwa na watanzania” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
“Wajibu wetu sasa ni kumuombea kiongozi wetu, wajibu wetu sasa ni kuyaenzi yale yote mazuri tunayoyafahamu” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Nae Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Kabudi amesema Mstaafu Mkapa amefariki baada ya moyo wake kusimama ghafla ukiandamana na Malaria.
“Hayati Benjamin Mkapa alikuwa Rais wa Kwanza kuchaguliwa chini ya mfumo wa vyama vingi ulioanzishwa 1992” Waziri Kabudi
“Hayati Benjamin William Mkapa, alifariki kwa ugonjwa wa Moyo kusimama ghafla (cardiac arrest), ulioandamana na Malaria, tarehe 23 Julai 2020, majira ya saa 3 na dakika 30 usiku akiwa na umri wa miaka 81” Waziri Kabudi