Wiki moja baada ya kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya watani zao wa jadi Dar es Salaam Young Africans, leo March 4 Simba wameikaribisha Mbeya City kucheza mchezo wao wa 24 wa Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Hii ni game ambayo kwa mujibu wa benchi la ufundi la Simba wanasema hawakuwa wakiichukulia poa hata kidogo, hiyo inatokana kuongoza Ligi kwa tofauti ya point mbili tu dhidi ya watani zao wa jadi ambao wako nafasi ya pili na kesho watacheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Leo Simba wamejikuta wakilazimishwa sare ya kufungana 2-2 dhidi ya Mbeya City, matokeo ambayo yanawafanya wafikishe jumla ya point 55 katika msimamo wa Ligi Kuu na kufuatiwa na wapinzani wao Yanga waliyo nafasi ya pili katika Ligi wakiwa na point 52, kama Yanga atashinda kesho dhidi ya Mtibwa Sugar atakuwa sawa na Simba kwa point.
Mbeya City ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 38 kupitia kwa Ditram Nchimbi, lakini Simba wakasawazisha goli hilo dakika ya 65 kupitia kwa Ibrahim Ajib, kabla ya Kenny Ally kuifungia City goli la pili dakika ya 78 lakini Shiza Kichuya aliisawazishia Simba dakika ya 86 kwa mkwaju wa penati.
ALL GOAL: SIMBA VS YANGA FEBRUARY 25 2017, FULL TIME 2-1