Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba leo Septemba 19 2016 imeandika barua kupitia kwa katibu mkuu wake Patrick Kahemele kueleza na kuomba kutoendelea kutumia uwanja wa Uhuru kwa sababu sio salama kwa afya za wachezaji, Simba wameandika barua hiyo na kueleza sababu 3 za wao kutotaka kuendelea kuutumia uwanja huo.
- Usalama wa afya za wachezaji kutokana na plastic za kushikia nyasi bandia kukauka hivyo kuwa hatarishi kwa afya za wachezaji kwa kuchubuka ngozi.
- Katika mechi kati ya Simba dhidi ya Azam FC mashabiki waliingia kwa tabu uwanjani kutokana na kuwa na msongamano, kwani nadhani kumeongezeka kwa watu Dar es Salaam na wapenzi wa mpira wanaopenda kuingia uwanjani.
- Kuna haja ya kuufanyia marekebisho uwanja huo kwa kuweka plastiki mpya katika uwanja huo kutokana na zile za mwanzo kuchoka na kwa sababu zilikaa muda mrefu bila kutumika.
Simba imeomba kutotumia uwanja wa Uhuru kwa sababu pitch yake inaumiza wachezaji hivyo wanaomba watumie Taifa. pic.twitter.com/tVdzSLsdcS
— millard ayo (@millardayo) September 19, 2016
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0