Huenda unaweza kufikiria ni utani au mkwara tu wa klabu ya Simba kwa shirikisho la soka Tanzania TFF, ila Asubuhi ya March 23, ukweli umethibitika, uongozi wa klabu ya Simba March 23 umefanya mambo mawili makubwa kwa ajili ya klabu yao.
Simba kupitia kwa afisa habari wake Haji Manara wameeleza msimamo wao kwa barua “TFF mara nyingi wanasema barua zetu hazijafika, ila hii nimeileta kwa mkono wangu kwa katibu, kama wasipofanya mabadiliko ya ratiba ya Ligi kuweza kufanya tuwe michezo sawa na Yanga na Azam FC, sisi hatuendelei kucheza” >>> Manara
“Kuhusu Banda uongozi umemuandikia barua na anatakiwa kujieleza, kwa kutoa sababu kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu na Simba, kutokana na kumgomea kocha Jackson Mayanja, na kugoma kuvaa jezi za mdhamini” >>> Manara
Bonyeza play kumsikiliza Haji Manara akielezea hapa
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE