Msimu wa 2015/2016 wa Ligi Kuu soka Tanzania ndio ulikuwa msimu ambao Simba wamepewa majina ya utani mengi zaidi kutoka kwa wapinzania wao wa jadi klabu ya Dar es Salaam Young Africans, hii ilitokana na kukubali vipigo mara katika mechi za mzunguuko wa kwanza na wa pili.
Leo May 22 2016 Simba imemaliza mechi yake ya 30 ya Ligi Kuu soka Tanzania bara kwa kucheza dhidi ya JKT Ruvu uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kukubali kipigo cha goli 2-1, mechi ya leo ilikuwa ni mechi ya 6 kwa Simba kufungwa katika mechi zake 30 ilizocheza msimu huu.
Baada ya kipigo hicho mashabiki na wapenzi wa timu hiyo walionesha kuumizwa na matokeo hayo, mmoja kati ya watu walioumia ni bilionea kijana Afrika Mohamed Dewji aliyeamua kutumia account yake ya twitter kuonesha hisia zake na matokeo ya timu hiyo “#Simba mnatunyima raha, tumechoka kutaniwa na kutukanwa mitaani”
Kama utakuwa na kumbukumbu nzuri Mohamed Dewji aliwahi kuomba kuinua Simba, ombi ambalo liliifanya klabu hiyo kuwa kwenye headlines kwa muda mrefu, Dewji pia March 24 2015 alitajwa na jarida la Forbes kama bilionea wa 24 Afrika kati ya mabilionea 29, lakini yeye ndio alikuwa bilionea kijana kuliko wote akiwa na utajiri unaofikia trilion 2.43 za kibongo.
ALL GOALS: SIMBA VS COASTAL UNION FA CUP APRIL 11 2016, FULL TIME 1-2
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE