Hatimaye hatua ya Makundi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi imemalizika kwa kushuhudia timu za Simba, Yanga, Mtibwa Sugar na URA ya Uganda zikitinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo. Mchezo wa Simba na JKU ndio ulikuwa mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.
Mchezo huo wa Kundi A ambao umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli 1-0, umemfanya Simba kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo na mshindi wa pili wa Kundi B ambaye ni timu ya Mtibwa Sugar. Wakati wapinzani wao wa jadi klabu ya Dar Es Salaam Young African watacheza dhidi ya URA ya Uganda.
Goli pekee la Simba lilifungwa dakika ya 65 na kiungo wake mahiri Jonas Mkude, baada ya kutumia vyema nafasi aliyoipata . Kwa matokeo hayo Simba itacheza Jumapili ya January 10 saa 16:15 dhidi ya Mtibwa Sugar, wakati Yanga watacheza siku hiyo dhidi ya URA ya Uganda saa 20:15. Kesho hakuna mchezo wowote wa Kombe la Mapinduzi.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.