Baada ya klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba kumuwinda kwa muda mrefu mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi aliyekuwa anaichezea klabu ya Vital’O ya kwao Burundi Laudit Mavugo, hatimae usiku wa August 3 2016 aliwasili Dar es Salaam na kukabidhiwa jezi namba 45 akiwa uwanja wa ndege.
Mshambuliaji huyo aliyekuwa anawindwa na Simba kwa zaidi ya miaka miwili bila Simba kufanikiwa kumsajili, ametua Dar es Salaam baada ya kushindwa majaribio katika klabu ya daraja la pili Ufaransa, Laudit anaonekana kukubalika na kupewa nafasi kubwa Simba, tofauti na washambuliaji wengine wa kigeni ambao bado Simba inawajaribu.
Baada ya kumfuatilia kwa zaidi ya miaka miwili, Simba SC imefanikiwa kumleta Laudit Mavugo raia wa Burundi. pic.twitter.com/cL0UMmA2Ym
— millard ayo (@millardayo) August 3, 2016
ALL GOALS: SIMBA VS COASTAL UNION FA CUP APRIL 11 2016, FULL TIME 1-2