Kama hukuwahi kubahatika kutembelea Singapore basi Marina Bay ni moja kati ya sehemu ambazo unapaswa kutembelea kama utafanikiwa kufika Singapore. Marina Bay ni uwanja wa mpira wa miguu ambao unaelea kwenye maji, yaani sehemu ya kuchezea inaelea ila majukwaa yapo nchi kavu.
Marina Bay umejengwa kwa vyuma lakini unaelea na unatajwa kuwa na uzito wa tani 1,070 ambazo ni sawa na uzito wa watu 9000, upande wa jukwaa la mashabiki lina uwezo wa kubeba watu 30,000. Uwanja huo toka mwaka 2007 umekuwa ukitumika kwa shughuli mbalimbali kama soka, michezo mingine, matamasha, maonyesho ya sanaa pamoja na sherehe za kitaifa zinazohusisha gwaride la askari jeshi na polisi.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata,pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE