Baada ya kusimama Ligi Kuu kwa wiki moja ili kupisha mechi za Kombe la FA, Ligi Kuu Tanzania bara mzunguuko wa pili umeanza kwa vilabu vya Ligi Kuu kurudi uwanjani leo January 30, uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, Simba walikuwa wenyeji wa African Sports wakati ambao watani zao wa jadi Yanga walikuwa Tanga kucheza na Coastal Union.
Simba walikuwa uwanja wa Taifa kurudiana na African Sports ambao mchezo wa mzunguuko wa kwanza uliochezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga September 12 2015 waliwafunga kwa goli 1-0. January 30 2016 African Sports walirudi tena kuvaana na Simba katika mchezo wa mzunguuko wa pili na kuchezea kichapo.
African Sports wameendeleza kuwa vibonde wa Simba baada ya kukubali kipigo cha goli 4-0, magoli ya Simba yalianza kufungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Hamis Kiiza dakika ya 14, Hassan Kessy dakika ya 31 na dakika ya 43 Hamis Kiiza alifunga goli la tatu kwa Simba, kabla ya Haji Ugando hajapachika goli la nne dakika ya 75 kipindi cha pili.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa January 30
- Coastal Union 2 – 0 Yanga
- JKT Ruvu 0 – 0 Majimaji FC
- Mwadui FC 1 – 0 Toto Africans
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.