Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema serikali yake itaimarisha mapambano dhidi ya magaidi wa al-Shabab mwaka 2024.
Akihutubia mkutano wa hadhara mjini Mogadishu Jumatano jioni rais Mohamud alieleza imani yake kwa vikosi vya usalama vya Somalia katika azma yao ya kuleta utulivu nchini humo.
Rais Mohamud alisema awamu ya kwanza ya operesheni inayoendelea nchini humo ya kuwaondoa magaidi wa al-Shabab imekamilika, akibainisha kuwa serikali inaandaa wanajeshi ambao wanafanya kazi maalum ili kuleta mafanikio yaliyopatikana katika maeneo yaliyokombolewa.
Rais Mohamud ambaye ameapa kupambana kwa kila hali na magaidi wa al-Shabab, alisema vikosi vya usalama vya Somalia vimeonesha weledi, nidhamu, na uaminifu katika kukabiliana na changamoto na vitisho vingi.