Meli ya Uturuki iliyobeba misaada ya kibinadamu kuelekea Somalia ilitia nanga Jumamosi katika bandari ya Mogadishu.
Meli ya iliyobeba tani 3,000 za msaada, ilisafiri Septemba, 29 kutoka Mersin katika jimbo la kusini la Türkiye na kupokelewa na maafisa wakuu wa serikali, akiwemo Naibu Waziri Mkuu Salah Jama pamoja na Kamishna wa Usimamizi wa Maafa Mahamuud Moallim katika hafla iliyofanyika bandarini.
Balozi wa Uturuki nchini Somalia Alper Aktas na wawakilishi kutoka mashirika ya misaada ya kibinadamu kutoka Türkiye pia walikuwepo.
“Msaada huo unajumuisha aina mbalimbali za vyakula, mahema, na mahitaji muhimu ya maisha, ambayo ni jumla ya tani 3,000. Msaada huu unalenga kuboresha kwa kiasi kikubwa hali ya maisha ya wale wanaohitaji,” Shirika la Kukabiliana na Majanga la Somalia (SoDMA) lilisema katika taarifa yake.
“Kama kawaida, Türkiye itaendelea kutoa mkono wake wa usaidizi kwa watu ndugu wa Somalia. Kuelekea mustakabali mzuri na watu ndugu wa Somalia,” Ubalozi wa Uturuki mjini Mogadishu ulisema katika taarifa.
Uturuki imewasilisha zaidi ya tani 60,000 za msaada tangu 2016 kwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki, ambayo inakabiliwa na majanga ya asili, ikiwa ni pamoja na ukame, njaa, mafuriko na vimbunga