Son Heung-min anasema alifikiria kuacha soka la kimataifa kufuatia msukosuko wa Kombe la Asia akiwa na Korea Kusini lakini akaamua kuendelea kwa ajili ya mashabiki.
Nahodha huyo wa Korea Kusini na Spurs alidokeza mashaka kuhusu mustakabali wake wa kimataifa mara tu baada ya kushindwa kwa mabao 2-0 na Jordan katika nusu fainali mwezi uliopita.
Baadaye iliibuka kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alicheza huku kidole chake kikiwa kimeteguka kutokana na kuchuana na mwenzake Lee Kang-in usiku wa kuamkia mchezo huo.
Jurgen Klinsmann, ambaye aliahidi kutoa Kombe la Asia la kwanza la Korea Kusini katika miaka 64, alifukuzwa kazi baada ya mwaka mmoja tu.
“Kuichezea timu ya taifa ni ahadi kati yangu na mashabiki,” Son aliwaambia wanahabari kufuatia sare ya Alhamisi ya 1-1 dhidi ya Thailand katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia.