Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kwa mujibu wa Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto ya Mwaka 2022, Mkoa wa Songwe unaongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha mimba za utotoni ukilinganisha na Mkoa mwingine wowote Tanzania.
Rais Samia amesema hayo wakati akizindua Ripoti hiyo ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania ya Mwaka 2022 na Ugawaji wa Magari ya Kubebea Wagonjwa na Vifaa Tiba Jijini Dar es salaam.
Rais Samia amesema “Sote tunao wajibu wa kulinda maisha ya Watoto wetu tutimize wajibu wetu, ripoti hii inaonesha kumekuwa na mafanikio katika kupunguza mimba za utotoni, kutoka 27% mwaka 2015/2016 hadi 22% mwaka 2022 tumepunguza kwa 5%”
“Tumeona Mikoa ya Dodoma, Kigoma, Tabora na Shinyanga imepunguza kiwango cha mimba za utotoni kwa kasi kubwa zaidi ikilinganishwa na Mikoa mingine ili ni jambo zuri na la kupongezwa hongereni kwa Mikoa hiyo”
“Mikoa inayoongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha mimba za utotoni ni Songwe (45%), Ruvuma (37%), Katavi (34%), Mara (31%) na Rukwa (30%)l