Hili ni miongoni mwa matukio ya Mike Sonko seneta wa Nairobi yatakayokumbukwa kwenye list ya matukio yake ya mwaka 2014.
Mike Sonko ni mwanasiasa maarufu nchini Kenya ambae mara nyingi amekuwa na muonekano wa kiujana zaidi au unaweza kusema ni kisharobaro zaidi…. Sonko ambae aliwahi kuwa mbunge na akaingia kwenye headlines za kuingia bungeni akiwa na cheni zake kifuani pamoja na hereni, bado anapenda kupendeza kwa kuvaa kofia, vito vya thamani, T shirts za kisasa, jeans na wakati mwingine kupaka rangi nywele zake.
Nyakati tofauti seneta huyu amehusishwa kwenye vituko mbalimbali ambapo kingine ni kile cha kumpigia simu Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kumuweka loudspeaker mbele za watu.
Kwenye moja ya mahojiano na kituo cha television Mike Sonko alisema kwamba alifanya hivyo ili waandishi wa habari wasikie kauli ya kiongozi wa nchi ambapo eneo hilo kulikua na nyumba zinabomolewa hivyo hakufanikiwa alipojaribu kuwatetea wananchi wake wasibomolewe nyumba ndio maana akaamua kupiga simu kwa rais mwenyewe ili awazuie polisi kuendelea kubomoa.
Video yenyewe ndio hii na mwisho wa siku Sonko alifanikiwa kusimamisha hiyo bomoabomoa.
Kama umeipenda hii stori na unataka kila cha millardayo.com kisikupite, unaweza kujiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Instagram facebook ili niwe nakutumia kila kinachonifikia.