Sophia Huang Xueqin na Wang Jianbing walihukumiwa kifungo cha jela nchini China kwa madai ya kuchochea uasi dhidi ya serikali.
Walishtakiwa kwa kuandaa mikusanyiko ya mara kwa mara ili kujadili masuala ya kijamii kama vile ufeministi wa wanawake, haki za LGBTQ+ na masuala ya wafanyakazi, kuchapisha makala ambayo yalionekana kuwa ya uchochezi kwa serikali, na kuandaa kozi za mtandaoni ambazo zilichochea kutoridhika na nchi.
Mamlaka ya Uchina iliwashutumu kwa kushambulia sifa ya serikali ndani na kimataifa