Afrika Kusini imewasilisha kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ya (ICJ) iliyopo The Hague Nchini Uholanzi dhidi ya Israel kwa kile ilichokitaja kuwa ni vitendo vya “mauaji ya kimbari” katika ukanda wa Gaza.
Kesi hiyo katika ICJ inahusiana na madai ya ukiukaji wa Israel wa jukumu lake chini ya mkataba wa mauaji ya kimbari na kusema kuwa “Israel imejihusisha, inajihusisha na inatishia kushiriki zaidi katika vitendo vya mauaji ya kimbari dhidi ya Watu wa Palestina huko Gaza”.
Katika kesi hiyo, Afrika Kusini pia inasema Israel imekuwa ikichukua hatua ‘’ kwa lengo la kuwaangamiza Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kama sehemu ya kundi pana la Taifa, rangi na kabila la Palestina
Hata hivyo Israel imepinga mashtaka hayo huku Msemaji wa Wizara yake ya mambo ya nje Lior Haiat akiandika yafuatayo kwenye ukurasa wa X ———> “Israel inakataa na kuchukizwa na kashfa inayoenezwa na Afrika Kusini na ombi lake’ kwa mahakama ya ICJ”