Korea Kusini ni moja ya Mataifa yaliyoendelea kiuchumi na raia wake hutumia masaa mengi zaidi kufanya kazi.
Utafiti uliofanywa na Shirikisho la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo OECD ulifanya uchunguzi na kugundua raia wa Korea Kusini hufanya kazi saa 2,163 kwa mwaka tofauti na raia wa Ujerumani ambao hutumia saa 1,388.
Kilichonifikia ni kwamba wafanyakazi katika ofisi mbalimbali katika mji mkuu wa nchini hiyo Seoul wamekuwa wakilipia pesa ya usingizi wakati wakipata chakula cha mchana ili kupunguza uchovu.
Kuna vyumba maalum kabisa vya kupumzika na hata kufanya massage ambavyo vimekuwa maarufu sana hasa katikati ya miji yenye ofisi nyingi.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE