Hii ni habari nyingine njema kabisa na ninakumbuka May 2 2017 niliweka stori ya Jamaa mmoja wa Kenya aliejishindia Shilingi za Kitanzania zaidi ya BILIONI 4 kwa sababu tu alitabiri na kupatia mechi 17 kwenye kampuni ya SPORTPESA.
Mimi kama Mwandishi wa habari nimekua nikifatilia sana pia habari za Kenya na kuna wakati niliona jinsi Betting kwenye SPORTPESA imekua ikifanywa kwa uwazi na kutajirisha watu lakini pia kuona wadau wa soka wanapelekwa Kenya kutokea Uingereza kutoa mafunzo.
Hayo yote nilikua nayaona Kenya na nikawa najiuliza ni lini watakuja na Tanzania, leo ghafla kwenye timeline ya Twitter naanza kuona Mtangazaji Salama Jabir, Ay na MwanaFA wanaandika kuhusu SPORTPESA kuja Tanzania nikafurahi.
Yule jamaa wa Kenya aitwae Samuel alishinda kiasi hiko cha fedha baada ya kutumia kama shilingi elfu 5 ya Tanzania kwenye machaguo mawili tofauti lakini akajishindia huo mzigo wote na sasa amekua miongoni mwa Wakenya ambao hawatausahau mwaka 2017.
Naomba kuchukua nafasi hii kuwaambia SPORTPESA karibuni Tanzania.
.
Nimeona timeline kwamba SPORTPESA wale wanaowapa Wakenya Mabilioni wameingia na Tanzania, I hope ni kweli, niko tayari kuripoti ?
— millard ayo (@millardayo) May 8, 2017
.
Sasa kupitia kwa Salama ndio nimeamini SPORTPESA wameingia TZ ?, kesho @TZSportPesa wapi nije kuchukua habari ? https://t.co/RYUfhKhj0P
— millard ayo (@millardayo) May 8, 2017