Wajumbe wa Jukwaa la Kibunge la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF) kwa pamoja wamekubaliana kumuunga Mkono Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, katika azma yake ya Kugombea nafasi ya Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).
Wajumbe hao Wakiongozwa na Rais wa SADC-PF ambaye pia ni Spika wa Seychelles, Mhe. Roger Mancienne, wamepitisha azimio hilo leo tarehe 6, Julai 2023 wakati wa kuhitimisha Mkutano wa 53 wa SADC-PF uliofanyika katika Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu Jijini Luanda, Nchini Angola huku kauli ya Dkt. Tulia ikiwa ni “Ufanisi, Uwajibikaji na Uwazi katika IPU”