Bado kuna mvutano ambao upo kuhusu ishu ya Mbunge Zitto Kabwe kusimamishwa uanachama wa CHADEMA ambapo uamuzi huo ulitokana na kuwepo taarifa kwamba kesi aliyofungua Mbunge huyo kupinga kuvuliwa uanachama ilikuwa imeondolewa Makahamani.
Zitto alienda kuwaaga wananchi wake wiki iliyopita jimboni kwake kwamba hatogombea tena Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, bado kuna mvutano juu ya namna ambavyo uamuzi wa Mahakama umetolewa.
Leo Kikao cha Bunge kimeanza, Spika wa Bunge la Tz, Anne Makinda amesema ishu ya Mbunge Zitto Kabwe kusimamishwa bado haijawafikia rasmi taarifa ya Mahakama kuhusu kufutwa kwa kesi yake.
“Kitu chenyewe kinachotokea ni kuarifu Tume ya Uchaguzi kwamba huyu mtu sasa hayupo.. Suala lenyewe lilikuwa Mahakamani, sisi lazima tupewe official communication“– Spika Anne Makinda.
#AMPLIFAYA #March172015 #1 ‘Ofisi ya Bunge haijapata barua ya Chadema kumfuta/kumzuia Zitto kuhudhuria vikao vya bunge’ – Spika Makinda.
— millardayo.com (@millardayo) March 17, 2015
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook