Wakiwa wanaongoza ligi kuu ya Hispania, mabingwa wa ulaya klabu ya Real Madrid November 22 2014 ilitupa karata yake ya 14 katika mchezo dhidi ya Eibar.
Wakiwa ugenini klabu hiyo chini ya Carlo Ancelotti imekaribia kuivunja rekodi ya Jose Mourinho aliyoiweka na timu hiyo kwa kushinda mechi 15 mfululizo, hii imekuja baada ya ushindi wao wa leo dhidi ya Eibar, ushindi wa 14 mfululizo kwenye mashindano yote.
James Rodriguez alianza kufungua ukurasa wa magoli kipindi cha kwanza katika dakika 23 kabla ya Cristiano Ronaldo kufunga goli la pili katika dakika ya 43 ambapo kipindi cha pili Karim Benzema akafunga goli la 3 dakika ya 69 kabla ya Ronaldo kufunga goli lake la pili kwenye mechi hiyo na kutimiza jumla ya magoli 20 kwenye la liga ndani ya mechi 12.
Mpaka mechi inamalizika Madrid walitoka na ushindi wa 4-0 na kuendelea kuongoza ligi hiyo.
Takwimu za Mechi
Eibar: Iruretagoiena Aranzamendi, Bóveda, Albentosa, Ekiza, Minero Fernandez, Errasti, García Carrillo, Capa, Arruabarrena (Lekic 78), Berjón Pérez (Lara Grande 78), Del Moral Fernandez (Rodríguez Díaz 70)
Subs not used: Añibarro, Nieto Vela, Boateng, Jiménez Merlo
Goals: NONE
Booked: Irureta 32, Arruabarrena 71, Errasti 81, Albentosa 82
Real Madrid: Casillas, Carvajal, Pepe, Ramos (Varane 73), Marcelo, Isco, Kroos, Rodríguez (Coentrao 78), Bale, Benzema, Ronaldo (Arbeloa 84)
Subs not used: Varane, Khedira, Navas, Hernández, Nacho
Goals: Rodriguez 23, Ronaldo 43, 83, Benzema 69
Booked: Ramos 21, Rodriguez 42