Sonda ya Dihlu–Nyota ya asubuhi ni kikundi cha watu saba kilichotengezwa kutokana na ujazo wa sauti nzito za wanaume zisizochujwa na vyombo vya studio bali ni sauti walizobarikiwa na Mungu, huku zikitengeneza midundo na kuimba kwa wakati mmoja.
Angalabu ni mara chache kukuta msanii akiimbia bila kutumia msaada wa vyombo mathalani Gitaa, Vinanda ama CD lakini vijana 7 wa kundi la Sonda ya Dihlu ama Nyota ya Asubuhi wamethubutu kufanya hivyo.
Ayo Tv na Millardayo.com imeweza kufanya mazungumzo na waimbaji wa kundi hili ambapo wanasema historia yao ilianzia mwaka 2006 na hadi sasa wana miaka 13, huku wakiwa wameanza chini ya watu Watano na hadi sasa wapo Saba.