Mataifa ya Marekani, Ufaransa na Uingereza yamefanya mashambulio wakilenga vituo vitatu huko Syria kama adhabu kwa madai kwamba utawala wa Rais Bashar al-Asad, ulitumia silaha za kemikali dhidi ya raia wake.
Taarifa zinasema milio ya mabomu imesikika katika maeneo kadhaa ya miji wa Damascus na Homs.
Taarifa iliyotolewa na rais Trump amedai kwamba vituo vilivyolengwa vinahusiana na utafiti wa uhifadhi na utengenezaji wa silaha za kemikali.
Rais Trump ameongeza kusema kwamba Marekani iko tayari kuendeleza mashambulio hayo hadi utawala huo wa Syria utakapoacha kabisa kutumia silaha za kemikali.
Naye rais wa Syria Bashar al-Asaad anasema kuwa mashambulio yaliotekelezwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa yamemfanya kuwa jasiri zaidi ya ilivyokuwa awali kukabiliana na wapinzani wake.