Watumiaji wa huduma za mawasiliano wanashauriwa kujihadhari dhidi ya utapeli kwenye
mitandao ya simu za mkononi kama ifuatavyo:
9. Usijibu ujumbe unaopokea kwenye akaunti yako ya barua pepe unaokutaka kuhakiki
taarifa zako.
10. Usijibu ujumbe wowote wa barua pepe unaokueleza kuwa umeshinda bahati nasibu.
11. Usitunge na kusambaza ujumbe wa maudhi, uzushi, uchochezi.
12. Usisambaze ujumbe wa chuki, maudhi, uchochezi unaopokea.
13. Usitembelee tovuti na blogu za ponografia/ ngono.
14. Tunza vifaa unapohifadhi kumbukumbu zako kama vile kompyuta, simu za mkononi, flash
disks na DVDs.
15. Ukifanyiwa uhalifu ambapo simu au mtandao vimetumika kufanyia uhalifu huo hilo ni kosa
la jinai. Toa taarifa Polisi haraka.
16. Ukipata matatizo kwenye matumizi ya mtandao, wasiliiana na kitengo cha Tanzania
Computer Emergency Response Team ( TZ-CERT) kwa barua pepe info@tzcert.go.tz
au ofisi yoyote ya TCRA.
17. Usipopata ushirikiano wa kutosha kwa mtoa huduma wako katika kutatua tatizo lako
wasilisha malalamiko yako TCRA. Unaweza kuwasilisha malalamiko kwa kutuandikia, kufika ofisini Dar Es Salaam au ofisi za Kanda na kupiga simu na kwa kutuma barua pepe – malalamiko@tcra.go.tz